Ni kweli usio pingika kwamba kuna njia nyingi sana za kutangaza biashara siku hizi, lakini kadri muda unavyozidi kwenda njia hizi zimekuwa zikipoteza umuhimu (kuisha muda wake) na kushindwa kutumiwa na watumiaji na wafanyabiashara wasasa.

Kuliona hili leo tunakuleta Loko Find, hii ni njia mpya kabisa ya kuweka biashara yako mbele ya wateja wengi zaidi na kisasa zaidi. Njia hii haijalishi kama wewe ni mjasiriamali mdogo au mfanyabiashara mkubwa au hata wa kati, kwani wote wanaweza kupata wateja kwa urahisi na haraka kupitia Loko Find.

Muonekano wa App ya Loko Find
Muonekano wa App ya Loko Find

Mbali ya kuwa ya kuwa Loko Find inakusaidia kukutana na wateja wengi zaidi, pia kupitia Loko Find unaweza kupata nafasi ya kutangaza biashara yako kwa haraka na kwa urahisi. Kuelewa zaidi hivi ndivyo Loko Find inavyofanya kazi.

Jinsi Loko Find Inavyofanya Kazi

Kuweza kuelewa kwa urahisi unaweza kufikiria Loko Find kama sehemu ya kukutana na wanunuzi pamoja na wauzaji, lakini hii sio kama sehemu ya kuuza na kununua bali hii ni sehemu ambayo wateja watapata nafasi ya kufahamu biashara husika kwa undani zaidi kabla ya kufanya biashara, hii inasaidia mteja kufurahia huduma na kurudia tena kufanya biashara kwa kuwa anafahamu biashara husika.

Pia hii inayo faida nyingi zaidi kwa mteja kutokana na kupata nafasi ya kufahamu biashara nyingi mbalimbali hivyo kufanya uamuzi sahihi wa kuchagua washirika bora wa kununua bidhaa au wakufanya biashara. Mbali ya hayo zipo faida nyingi sana kwa mteja na mfanyabiashara ambazo nitakueleza baadae kidogo.

https://youtu.be/inMRJlmpPs8

Je Loko Find ni nini.?

Loko Find ni sehemu pekee ambapo wajasiriamali wote wa kitanzania wataweza kuweka aina zote za biashara zao pamoja na mawasiliano yako kwa ajili ya wateja kuweza kuwasiliana nao pale wanapo hitaji kupata huduma au kufanya biashara.

Loko Find inafanya kazi kwa kuangalia zaidi eneo ulilopo hii inasaidi kusogeza huduma karibu zaidi na kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka kwa mfanyabiashara kwenda kwa mteja. Kupitia Loko Find utaweza kujua aina zote za biashara zilizo karibu na wewe bila kujali eneo ambalo unapatikana kwa sasa.

Kwa mfano kama unatafuta sehemu za huduma ya chakula na upo sehemu ambayo huwenda uhifahamu vizuri basi unaweza kufungua Loko Find na kuona biashara zote za chakula zilizopo karibu na eneo unalo patikana kwa muda huo.

Hiyo haishii hapo, utaweza kuwasiliana na biashara usika kwa urahisi kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi ndani ya Loko Find na moja kwa moja utaweza kuwasiliana na biashara husika kwa urahisi na haraka.

Loko Find  ni Rahisi Kutumia 
Loko Find  ni Rahisi Kutumia 

Mbali ya hapo utaweza kuona ofa mbalimbali za biashara husika, hii ikupa nafasi ya kuweza kupata huduma bora kwa bei nafuu zaidi.